Al-Iman Society of Northamptonshire

Login   |    Signup  |

Vipi Dss Inaweza Kusaidia

Mtu yeyote anaepata msaada na ana kipato kidogo anaweza kupata msaada wa gharama za mazishi. Msaada unaweza ukawa gharama kamili au baadhi yake kwa ajili ya gharama za mke/patna, mtoto, jamaa wa karibu au rafiki ikiwa msimamizi wa mazishi au mke/patna atasimamia mazishi na anapata moja ya misaada ifuatayo:

- Income support – Ikiwa hawezi kufanya kazi na anasaidiwa kujikimu

- Income based Jobseeker’s Allowance – Anaesaidiwa kujikimu wakati bado anatafuta kazi na hajapata na yumo kwenye daftari la wanaotafuta kazi.

- Housing Benefit- Anaepata msaada wa kulipiwa baadhi ya kodi ya nyumba kutokana na kuwa na kipato – mshahara usiokidhi mahitaji yake.

- Council Tax Benefit – Anaepata msaada wa kulipiwa baadhi ya kodi ya Council kutokana na kuwa na kipato – mshahara usiokidhi mahitaji yake.

- Working Families’ Tax Credit – Mkopo wa kodi kwa familia zinazofanya kazi na kuwa na kipato kidogo.

- Disable person’s Tax Credit – Mkopo wa kodi kwa wenye vilema.

- Umesimamia mazishi ya marehemu lakini huna gharama kamili za kulipia

DSS ina utaratibu wa kufuatilia kwa karibu kama marehemu alikuwa na akiba yoyote kabla ya kutoa uamuzi wa kuchangia na kiwango cha kusaidia. Hivyo:

- Hutazama kama kulikuwa na akiba kwenye Akaunti za marehemu.

- Hutazama kama kuna Bima ya aina yoyote ilikuwa ikilipiwa na marehemu au malipo ya mazishi yanayolipwa kabla.

- Hupitia kwenye vilabu vya mazishi (funeral clubs) kama marehemu aliwahi kujiunga nazo.

- Huangalia kama marehemu alikuwa akitoa michango inayoweza kupatikana kutoka kwenye asasi za kujitolea (Charities – kama ulivyo mfuko wetu wa misiba).

- Huangalia kama jamaa wa marehemu wanaweza kuchangia chochote.

Sheria ya nchi inasema gharama za mazishi zitolewe kwenye mali za marehemu kabla ya kitu chochote kulipwa (Sheria ya dini ya kiislamu pia inasema hivyo hivyo). Hivyo DSS baada ya kulipia gharama inaweza ikazidai fedha hizi kutoka kwa wafiwa ikibainika kwamba marehemu alikuwa na mali, nyumba, ardhi, hisa, akiba, au anadai sehemu na kadhalika. Hii ni kwa sababu inawezekana marehemu kuwa na kiakiba lakini kikajulikana baada ya kufariki kwake.

Malipo hulipwa kwa mara moja kwa njia ya cheki ambayo utatakiwa kumkabidhi mkurugenzi wa mazishi na utatakiwa kuwasilisha maombi katika kipindi kisichozidi miezi mitatu tokea kuzikwa marehemu.

Ukitaka kuomba utatakiwa kujaza fomu SF200 ambayo inapatikana Jobcentre au katika tovuti www.jobcentreplus.gov.uk.

Timu ya misiba itasaidiana na jamaa wa wafiwa katika kufuatilia kama mwenye kusimamia mazishi ataweza kuwa na sifa za kuomba msaada kutoka DSS.

 

Waislamu watakuwa na dhimma kwa kushindwa kutekeleza jukumu lao la Fardhi

 

Gharama za mazishi zinabaki kuwa deni lenye kuongezeka kwa riba (interest) kama halijalipwa kwa muda uliowekwa

 

Uchunguzi wa maiti unaweza kupendekezwa na madaktari kujua sababu ya kifo lakini itakuwa bora zaidi kama hautofanyika kwani utachelewesha taratibu za mazishi na Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam amependekeza kuharakishwa kwa maziko.