Al-Iman Society of Northamptonshire

Login   |    Signup  |

Mfuko hautohusika na mambo mengine anayofanyiwa maiti na si ya lazima kama khtima, arubaini, kulisha chakula, na kusafirisha mwili wa marehemu nchi nyengine n.k

- Mfuko hautojumuisha jamaa wa marehemu ambao hawaishi nae ( kama wanaishi nchi nyengine). Hata hivyo kama kukitokea msiba kwa jamaa wa karibu, wataweza kumsaidia muislamu mwenzi wao kwa njia ya michango.

- Mkurugenzi wa Mazishi atakabidhiwa cheki na si fedha taslimu isipokuwa tu kama wafiwa tayari wameshalipia gharama za mazishi, gharama hizi watapewa wafiwa.

- Utafiti utafanyika kuhakikisha Kama mchangiaji alikuwa akipokea msaada kutoka serikalini kama DSS au income support ili mfuko kuweza kujua utaweza vipi kuchangia.

Akaunti za marehemu hufungwa na kuzuiwa ikipatikana taarifa ya kufariki mpaka apatikane jamaa wa karibu mwenye kusimamia mambo ya marehemu

Mambo Muhimu Ya Kuyajua