Al-Iman Society of Northamptonshire

Login   |    Signup  |

Kila mchangiaji atatakiwa azingatie yafuatayo:

 

 

 

1 Kuhakikisha anachangia £5.00 kwa mwezi kwa mujibu wa makubaliano na mfuko.

2 Kuhakikisha anachangia kwa wakati na kupewa risiti kwa kila mchango atakaoutoa kwa ajili ya kumbukumbu.

3 Kila baada ya miezi sita atapata taarifa ya michango yake

4 Mchangiaji alieshindwa kutoa michango yake kwa miezi sita mfululizo atapelekewa barua ya ukumbusho na atahitajika kutoa maelezo ya sababu za kushindwa kuchangia.

5 Kamati ya nidhamu ya mfuko itakaa kujadili sababu hizo na kutoa maamuzi muafaka kama ni kuendelea kwa makubaliano maalum au kumfuta na kumtaarifu mhusika kwa maandishi.

6 Mchangiaji anaweza kujitoa katika mfuko kwa kutoa notisi kwa maandishi na sababu za kufanya hivyo kwa ajili ya kumbukumbu

7 Mchangiaji aliyejitoa akitaka kurudi tena kuchangia atatakiwa kujaza fomu mpya ya usajili

8 Kwa mchangiaji aliyefutwa kwa sababu ya kutokuchangia, ataruhusiwa kujiunga tena endapo atakubali kulipa malimbikizo ya michango yake iliyopita kwa makubaliano kati yake na mfuko

9 Michango iliyotolewa hubakia kwenye mfuko hata kama mchangiaji amejitoa au kufutwa au kuhama.

10 Ikiwa mchangiaji au wanaomtegemea atafariki nje ya Uingereza, mfuko pia utakuwa na jukumu la kuchangia gharama kwa sababu ya kutengwa fedha hizi kwa madhumuni haya . Kiwango kitaamuliwa baada ya kupata taarifa za gharama zilizotumika kutoka kwa jamaa wa marehemu.

11 Kukitokea kufariki kwa wategemezi wanaoishi nje ya Jimbo, mfuko utakuwa na jukumu la kuchangia gharama za mazishi tu lakini hautashiriki katika taratibu nyengine za kusimamia ila itaweza kutoa ushauri ukihitajika

12 Mgeni anaetoka nje ya nchi atakaefikia kwa mchangiaji atahesabika kama ni mtegemezi kwa muda wa miezi sita. Mchangiaji atapaswa kuutaarifu mfuko

13 Mchangiaji ana haki ya kupeleka malalamiko au dukuduku juu ya mwenendo wa mfuko au kutoridhishwa na jambo linalohusiana na mfuko kwa Amiri wa mfuko wa misiba na kama hatoridhishwa suala litapelekwa kwa Amiri wa Al-Iman.

14 Kwa wachangiaji wasio wakaazi watakuwa na masharti na taratibu za ziada

Taratibu Ya Masharti