Al-Iman Society of Northamptonshire

Login   |    Signup  |

Nafasi Ya Mfuko

Mfuko una nafasi muhimu katika jamii kwani unajenga umoja na moyo wa kushirikiana na kusaidiana katika wakati mgumu wa mitihani ya kuondokewa na jamaa zetu hasa katika nchi hii ambapo tupo mbali sana na ndugu zetu, wazazi, jamaa na marafiki hivyo:

 

 

 

Husaidia katika kuelewa taratibu za kufuatilia baada ya kufiwa na nini cha kufanya baada ya kufiwa.

 

 

 

Hutoa msaada wa kihali, kimali na kisaikolojia kwa wafiwa kuweza kukabiliana na majukumu mazito na kuwa pamoja kwa muda wote wa maombolezo.

 

 

 

Husaidia wasiokuwa na uwezo wa kulipa gharama za mazishi kwa ujumla au baadhi yake bila ya kubebeshwa mzigo wa deni linaloongezeka kwa njia ya riba ambayo ni haramu kisheria.

 

 

 

Hugharamia gharama za mazishi kwa mchangiaji na kwa wasiochangia utaweza kusaidia kwa asilimia isiyozidi 25% kutegemea na hali zao kiuwezo na hali ya kifedha ya mfuko.

 

 

 

Hutoa taarifa za maendeleo ya mfuko kila baada ya miezi sita na kuainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

 

 

 

Hutoa ripoti kamili ya mfuko kila mwaka na kuwapatia wote waliochangia