Forum Posts

Al-Iman
Sep 02, 2018
In Mafundisho
Imekusanywa na Muhammad Faraj As-Sa’ay Utulivu (Tumaaniynah) Utulivu (Tumaaniynah) ni nguzo muhimu sana katika nguzo za Swalah, na bila ya utulivu Swalah haiwi kamilifu. Siku moja Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa amekaa Msikitini, akaingia mtu mmoja na kuswali. Baada ya kumaliza akainuka na kwenda kumsalimia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swallah Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamuambia: “Rudi kaswali tena, wewe bado hujaswali.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) alimrudisha mtu huyo mara tatu, na kila anapomaliza kuswali alikuwa akimuambia: “Rudi kaswali tena, wewe bado hujaswali”. Yule mtu akamuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam): “Sijui kuswali vizuri kuliko hivi, (bora) nifundishe”. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) akamuambia: “Unapotaka kuswali tia udhu, kisha elekea kibla, kisha soma utakachoweza kusoma katika Qur-aan, kisha rukuu mpaka utulie (Tumaaniynah) na uwe na uhakika kuwa umerukuu (sawa), kisha inuka usimame sawa sawa (Tumaaniynah), kisha usujudu mpaka utulie (Tumaaniynah) na uwe na uhakika kuwa umesujudu sawa, kisha kaa vizuri mpaka utulie katika kikao chako (Tumaaniynah), kisha sujudu na utulie (Tumaaniynah) mpaka uwe na uhakika kuwa umesujudu sawa, kisha ufanye hivyo hivyo mpaka umalize kuswali”Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah Hadiyth hii na nyingi kama hizi zinatujulisha kuwa Swalah haiwi kamili bila ya utulivu (Tumaaniynah). Nako ni kutulia katika kila kitendo cha Swalah. Mtu anatakiwa atulie mpaka awe na uhakika kuwa ametulia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amempa jina la ‘Mwizi’ mtu anayeswali bila utulivu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Katika wezi wabaya kabisa ni wale wanaoiba katika Swalah zao, hawarukuu kwa ukamilifu wala hawasujudu kwa ukamilifu na hawawi na khushuu.” Na katika riwaya nyingine amesema juu ya ‘Mwizi wa Swalah’: “Na wala haunyoshi mgongo wake sawa pale anaporukuu na anaposujudu.” Imaam Ahmad, Al-Haakim na imesahihishwa na Imaam Adh-Dhahabiy. Kudokoa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza kudokoadokoa katika Swalah. Kwa sababu anayeswali kwa pupa bila ya utulivu anakuwa mfano wa kuku anayedokoa mtama, na huwa haipi haki yake Swalah, wala hakipi kila kitendo haki yake. Bali hampi Mola wake haki Yake. Kumbuka kuwa ndani ya Swalah yanapita mazungumzo baina yako na Mola wako (Subhaanahu wa Ta’ala). Katika Hadiyth ambayo sehemu ya mwanzo yake ni Hadiyth Al-Qudsiy, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Mwenyezi Mungu Anasema; ‘Nimeigawa Swalah baina yangu na baina ya mja wangu sehemu mbili, na mja wangu (ninampa) anachoniomba’. Mja anaposema: "الشوق للوهو ربوو الجلالومينو" MwenyeMungu Husema: “Mja wangu amenishukuru” Na anaposema: "الرومنسم الرومى" ، Mwenyezi Mungu Husema: “Mja wangu amenipa sifa yangu”. Na anaposema: “ مَلَهُو يَوْمُو الدُّنُو”, Mwenyezi Mungu Husema: “Mja wangu amenitukuza”, au Husema:“Mja wangu amejisalimisha kwangu ”. Na anaposema; يوريوآكَ نَتَبُ وُيَيَاوَكَ نَوْرَوِنِي”, Mwenyezi Mungu Husema: “Haya ni baina yangu na baina ya mja wangu na mja wangu atapata atakachoniomba.” Na anaposema: اهنؤوا الزورواتا المعزوفيمو. زهورهم الُنَوَنَ أَلْنَوَوَ فَلِيَوْمُ شَيْئُو الْمُضَغِّلُ فَلْيُوْمُوْم وَلَا الأَوَاوِيُّ ”. Mwenyezi Mungu Husema: “Hii ni ya mja wangu na mja wangu atapata anachoniomba” Mtu anapozungumza na mzee wake au mkubwa wake wa kazini au anapozungumza na mfalme katika wafalme wa dunia, huzungumza naye kwa heshima na utulivu kubwa. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) Anastahiki zaidi heshima na utulivu huo kuliko viumbe hao dhaifu. Mmoja katika Maulamaa amemfananisha anayeswali kwa pupa bila ya utulivu kuwa ni sawa na mwenye kunywa dawa chungu anapoweka chungwa lake tayari apate kula mara baada ya kunywa dawa kwa ajili ya kuuondoa uchungu wa dawa. Lakini yule anayestarehe ndani ya Swalah yake, mfano wake ni mfano wa mtu anayekunywa kinywaji kitamu. Anakunywa taratibu, akistarehe nayo huku akitamani kinywaji hicho kisimalizike. Mtu anapomjua Mola wake, na kuzijua neema alizopewa, kisha akaujuwa uwezo wa Mola wake juu yake, huyo ndiye anayemjua Nani anayemuabudu, na anampa heshima anayostahiki. Ibn al-Qayyim amepiga mfano wa mtu anayemuabudu Mola wake bila ya kumpa heshima anayostahiki kuwa ni mfano wa panya aliyemuua ngamia, kisha akamchukua ngamia huyo na kumpeleka penye tundu lake (tundu la panya) na kumtaka mkewe (ngamia) aingie ndani humo. Ngamia akamwambia panya: “Sikiliza bwana, nitafutie nyumba kiasi changu, au tafuta mke kiasi chako” ibn al-Qayyim alimaliza kwa kusema: “Na hivi ndivyo ilivyo, mtu ama amuabudu Mwenyezi Mungu kama Anavyostahiki kuabudiwa, au atafute kijiungu chake akiabudu kama anavyotaka yeye.”
0
0
28
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Cheese (Jibini) 250g Delicate dill (ni aina ya majani ambayo huleta harufu nzuri kwenye chakula kama ilivyo nanaa na kotmiri. angalia kwenye picha) Mayai 5 Unga wa ngano magi 4 Chumvi Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Single cream au double cream 300ml Siagi 250g Namna ya kutayarisha na kupika Changanya unga, siagi na baking powder pamoja na chumvi. Kata kata delicate dill uchanganye kwenye unga. Ikate Jibini kwenye chombo cha kukatia - Grater na kisha itie kwenye unga. Yachanganye mayai na  cream  uyachape  vizuri.   Anza kumimina mchanganyiko wa cream na mayai kwenye mchanganyiko wa unga. Utapata mchanganyiko uliokuwa  laini  lakini  unaweza  kusukumika.  Weka  unga  mkavu  kwenye  kibao  cha  kukatia  usukume  na  kata  shepu  uipendayo. Zipange kwenye tray ya kuchomea. Paka yai juu ya scones. Zichome  kwa  muda  wa  dakika  25 to 30 kwa  gas  mark 5. Zikiwiva ziache  zipoe  na  tayari  kwa  kuliwa. Kidokezo Scones  unaweza  kuzifanya kwa  shepu uipendayo, hasa  watoto  ni chakula wanachokipenda na  ni  kizuri  kwa  afya  yao  kwa  sababu  ya jibini. Pia kwa  kupata  rangi  nzuri  ya kupendeza  paka yai  lilochanganywa   na double  au single  cream
0
0
12
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Siagi 250g Sukari 250g Arki rose kijiko 1 cha  chai Zabibu 100g Unga wa ngano 100g Mayai 6 Baking powder kijiko 1 ½ cha chakula Namna ya kutayarisha na kupika Changanya siagi na sukari mpaka  ichanganyike vizuri. Weka  mayai  kwenye  mchanganyiko  wa  siagi  na  sukari. Tia arki. Changanya unga na baking powder. Utie  unga kwenye  mchanganyiko  wa  mayai, siagi sukari  kidogo kidogo mpaka  uone haukushiki  mikononi. Ipake siagi au mafuta   sahani ya kuokea - tray na uzipange rock cake.  Zichome  kwa  gas  mark 5  mpaka  ziwe  na  wekundu  wa kupendeza. Kidokezo Jitahidi  zisikauke   na zikaungua  sana  zitakuwa  ngumu  na  kila  zikikaa zinazidi  kuwa nzuri.
0
0
14
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Mchele vikombe  3 Kuku mgumu  1 Thomu/tangawizi ya  kusaga  vijiko  3 Mdalasini  wa  unga  vijiko  2  vya  chakula Kotmiri kishada  kimoja Mbatata 4 kubwa Zabibu kavu Vitunguu  maji  10  vikubwa Bizari nzima vijiko  4 vikubwa (uzile) Chumvi  kiasi Mafuta ya kupikia Magi vipande  viwili Namna  kutayarisha  na  kupika · Teleka  kuku na umtie  chumvi pamoja  na  mchanganyiko wa   thomu  na  tangawizi na  mdalasini muache  awive  lakini  umbakishe  na  supu  kiasi  ya  magi  1. · Chambua  majani  ya  kotmiri  uyaoshe  na  uweke  pembeni. · Kaanga  vitunguu maji  viwe  rangi  ya  zaafarani (golden  brown). · Menya  mbatata  na  uzikaange  ziwe  rangi ya  zaafarani(zikate  vipande  vidogo vya kiasi) Namna  ya  kutayarisha  wali na kuchanganya · Roweka  mchele  kwa  maji  ya  baridi kwa  dakika  5 · Teleka  sufuria ya  maji  ya  wali  na  utie  uzile uchemkie  pamoja · Uzile ukisha  toa  rangi, utowe  kwa  kichujio  cha  chai  na  weka  mchele uchemke mpaka  ukiukata  uwive  kiasi (ukiubinya  kwenye  mwiko ukatike. · Uchuje  wali maji  na  tayari kuuchanganya. · Weka  mafuta  uliyokaangia  vitunguu  kwenye  sufuria  kiasi  kijiko  1  cha  kula · Weka  wali robo  chini  ukifuatiwa  na  kuku  na  supu  yake   kiasi. · Tandaza  kotmiri  nuru zabibu  kiasi  na  funik a  kwa  vitunguu  vyako   ulovikaanga nusu ·Endelea  kutia  wali  wako  na  kuufuata  mfumo  huo  huo  na  ukimaliza  kwa mbatata  na  vitunguu ·Malizia  kwa  kuufunika  kwa  wali  uliobakia  na  nyunyiza  vijiko  3  vya  mafuta uliyokaangia  vitunguu. · Funika  foil na mfuniko  ili mvuke  usitoke  na  uweke  kwenye  moto  mdogo  mdogo uwive  vizuri  kwa  dakika  45. · Ukipendelea  kutia  kwenye  oven  pia  utawiva  vizuri  tu. Kidokezo Ni  wali  wenye  ladha  nzuri  na  harufu  ya  kuvutia  ukiupatia  saladi  na  ndizi  mbivu unapendeza  zaidi.
0
0
13
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Unga wa  ngano  kilo 1 Hamira vijiko  2   vya  kulia  chakula Chumvi Ufuta Siagi ¼  kilo Samli aina  yoyote  vijiko  2  vya  kulia  chakula Mayai 5 Maziwa magi 1 Namna  ya  kutayarisha  na  kupika · Changanya unga kwa kutia maziwa, siagi, mayai, chumvi na  hamira. · Ili ukandike  vizuri  unaweza  kuongeza  maji.  · Unga  ukishakandika,  weka  samli  na uukande  kidogo. · Kata  madonge  kwa  shepu  uipendayo  au  tumia  vibati  vya  kuchomea  mikate. · Weka  ufuta  juu yake  na  uwache  uumuke  vizuri. · Choma  kwenye  oven  kwa  gas  mark  5 au  umeme  250 · Baada  ya  dakika  10  itakuwa   tayari  ishawiva, lakini  pia  inategemea nguvu  ya oven. Kidokezo · Ni  mizuri  kwa  chai  ya  maziwa  au  ya  rangi (chai kavu)
0
0
27
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Makaroni ½ kilo Kuku au nyama ¼ kilo Tangawizi na thomu(iliyosagwa-paste) kijiko1 cha chakula Pilipili manga iliyosagwa ½ kijiko cha chakula Ndimu 1 Chumvi Unga wa  mahindi (fine corn flour) vijiko 3 vya chakula Mozarella cheese ½ kilo Tungule(Tomato/Nyanya) 3 Kitungu maji 1 Mafuta ya kupikia vijiko 2 Tungule ya kibati kijiko 1 cha chakula (tomato puree) Pili pili ya unga kiasi Namna Ya Kutayarisha  Na  Kupika · Mkate kuku vipande vidogo vidogo na umuoshe vizuri. · Mchemshe  kwa  thomu, tangawizi, chumvi na ndimu pamoja pilipili manga na ya unga ili apate kukolea vizuri  na kisha umuweke  pembeni. · Weka  maji  magi moja kwenye sufuria na kisha utie chumvi na pilipili manga kidogo na unga wa mahindi na uanze kupika uji wa gravy na hakikisha  usiwe mwepesi sana na uwe mzito wa kiasi. · Katakata kitunguu na umenye tungule (nyanya/tomato) ukaange mchuzi lakini bila ya kuunguza vitunguu na umalizie kwa kutia chumvi na nyanya puree. Pia hakikisha mchuzi huu usiwe na maji mengi ninachokusudia uwe dikodiko. · Yachemshe  makaroni  mpaka yawive  vizuri. · Weka makaroni kwenye tray ya kuchomea kwa kuyapanga makaroni nusu kwanza na kuweka kuku kidogo kisha mchuzi pamoja na gravy kwa kumalizikia na cheese. · Endelea kufanya mfumo huo kwa juu yake tena na tayari kwa kuyachoma kwenye oven gas mark 8. · Yafunike Makaroni kwenye foil kwa dakika 10 ili cheese iyayuke na baadae yafunue na kuyaacha kwa dakika 5 ili uipate rangi nzuri ya wekundu mwanana. Kidokezo Unaweza kuongeza mboga mboga uzipendazo ili kukifanya chakula kiwe na afya na lishe zaidi.
0
0
13
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Kebichi (Cabbage) 1 Kitunguu maji 1 Mbatata 2 za kiasi Tungule 2(nyanya) Bilingani 1 Pilipili mboga 1 Carrot 2 Chumvi Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya kulia chakula Bizari ya manjano Bamia vidole 7 (ukipenda) Namna ya kutayarisha na kupika · Likate kebichi na uliweke pembeni. · Zimenye mbatata na uzikaange pamoja na bilingani, bamia na uziweke pembeni(unapokaanga visiwe vyekundu sana) · Injika sufuria na uweke mafuta kiasi na ukaange kitunguu maji · Kabla hakijawa chekungu weka bizari, koroga kiasi ya sekunde 5 na katia tungule huku ukikoroga. · Koroga kidogo na uweke mboga ya kebichi pamoja na carrot, pilipili mboga ambazo utakuwa umezikata kata. · Punguza moto na uwache mboga iwive kwa mvuke. · Baada ya dakika 5 changanya mbatata na bilingani na uwache ikauke ila isiwe na maji mengi Kidokezo Mboga hii ina afya sana kwa sababu unaipika kwa mvuke pia unaweza kuongezea mboga mboga nyengine ili uipambe zaidi kwa afya bora. Usisahau kuweka chumvi
0
0
7
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Mchele magi 2 Nazi ya cream ½ au ya kibati 1 Hamira kijiko 1 ½ cha kulia chakula Hiliki iliyosagwa ¼ kijiko cha chai Ute wa yai 1 Maji ya vuguvugu magi 1 ikiwa utatumia nazi ya maji ya kibati na magi 2 ikiwa utatumia nazi ya kipande (cream coconut) Sukari ¼ kikombe cha chai Mafuta kidogo ikiwa yatahitajika wakati wa kuchoma chila Namna ya kutayarisha · Roweka mchele kwenye maji kwa masaa kumi. · Saga mchele kwa kutumia blender na uchanganye vitu vyote nilivyoviorodhesha hapo juu isipokuwa ute wa yai tu. · Hakikisha vimesagika vizuri (mchele usiwe na chenga nyingi). · Weka ute wa yai na usage tena kidogo tu. · Uwache unga uumke. Namna ya kupika · Tumia chuma kisichogandisha (non stick). · Chota mchanganyiko kwa upawa au kijiko chenye uvungu wa kiasi cha chuma utachotumia kuchomea. · Injika chuma ili kipate moto na uweke kijiko kimoja cha upawa na ufunike mpaka iwive vizuri au (ikauke) · Itowe uiweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa ikiwa unapenda kula vitu vya moto na ikiwa laa isubiri ipowe Kidokezo Kuwa makini kwa kutumia moto mdogomdogo  kwa kuchomea chila kwa kuhofia zisiunguwe na juu zikawa mbichi (Ili kuipata chila laini na mwanana lazima unga uwe laini na usiwe mzito kama wa vitumbua au mkate wa mchele).
0
0
8
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Tungule  2 Tango 1 Vitunguu maji vyekundu 3 Kotmiri ½ kicha (bunch) Parsley ½ kicha (bunch) Chumvi kiasi Carrot 3 Pili pili mboga ya njano na nyekundu 1 Celery vijiti 4 Ndimu kiasi Namna Ya Kutayarisha Na Kutengeneza Zioshe mboga mboga za kachumbari kwa maji ya vuguvugu Zikatekate zote kwa pamoja na uziweke kwenye mashine ya kusagia (Food Processor) Isipokuwa ndimu tu ndio utakuja kuiweka mwisho Zisage kwa kutumia numbari mbili kwa kusita kwa kila sekunde 1 mpaka kachumbari ichanganyike vizuri. Ikishanganyika, weka maji ya ndimu na itie kwenye bakuli tayari kwa kuliwa. Kidokezo Pendelea kuosha mboga mboga za saladi kwa kutumia maji ya moto (lakini si ya kuwivisha) ili kuuwa vijidudu. Pia usisage kwa muda mrefu ili kuepuka kuwa na maji mengi.
0
0
5
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
Vinavyohitajika Vipapatiro vya kuku (wings) robo kilo. Chumvi. Pilipili manga kijiko1 cha chai. Bizari nzima iliyosagwa kijiko1 cha chai. Paprika vijiko 2 vya chakula. Tangawizi na thomu iliyosagwa kijiko kimoja cha chakula. Ndimu moja nzima kubwa na yenye maji ya kutosha. Mdalasini uliosagwa kijiko 1 cha chai. Namna ya kutayarisha na kupika Visafishe vizuri vipapatiro na kisha vioshe. Viweke kwenye bakuli la kuwachanganyia huku umevigida maji vizuri. Weka viungo vyote kwa pamoja uvichanganye vizuri. Vikishachanganyika, vikamulie maji ya ndimu na uvichanganye tena vizuri. Vitie kwenye baking tray na uvichome kwenye grill huku ukivigeuza geuza mpaka viwive na viwe na rangi ya hudhurungi. Weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Kidokezo Ukiwa mpenzi wa pilipili utaongeza, pia unaweza kuvitia maziwa ya kuganda(mtindi) vijiko vinne vya chakula wanazidi ladha nzuri zaidi.
0
0
6
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Mapishi
📷 Vinavyohitajika Mchele 1 kg Vitunguu maji 1kg Mbatata 4 kubwa Thomu na tangawizi iliyosagwa vijiko viwili vya kulia chakula Kuku mmoja au nyama kilo moja Zabibu kavu ¼ kg Bizari nzima unga vijiko 2 vya chakula Mdalasini wa unga vijiko 2 vya chakula Chumvi Mafuta ya kupikia Magi ya chakula (kijani /zaafarani) Namna ya kutayarisha na kupika Chemsha kitoweo kwa thomu na  tangawizi,  bizari nzima  na  mdalasini. Kikishawiva weka pembeni (bakisha supu kiasi). Menya  vitunguu  maji  uvikate  na uvikaange  mpaka  viwe  na  rangi  nzuri ya  wekundu. Zimenye mbatata  na uzikaange pia  mpaka  ziwe nyekundu Roweka  mchele  kwa  muda  wa dakika  10 (lakini  inategemea  mchele  unaotumia, mchele  huu  ni basmati) Teleka maji ya kupikia wali na weka chumvi kiasi Subiri maji yachemke na kisha weka mchele. Uwache uchemke mpaka ukiuvunja  kwa  kidole  uwe unagawanyika.  Umwage maji.  Weka mafuta uliyokaangia vitunguu vijiko viwili vya chakula kwenye  sufuria. a.Weka wali kiasi b.Weka kuku na  supu, vitunguu, mbatata  na  zabibu  Fuata  mfumo  huo  kwenye  awamu  mbili  ya  wali na mwisho  nyunyiza mafuta  kiasi  ya robo  kikombe  cha  chai na  pia  ni  wakati  wa  kuzitia  rangi kwenye  sehemu  tafauti. Funika  foil  na  mfuniko juu ya wali  na  uweke  moto  mdogo  kwa  muda  wa  dakika  45 Ufunuwe  na  uuchanganye  vizuri  uupakuwe  na  tayari  kwa  kuliwa
0
0
82
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
KUNUIA HAJJ NA UMRA Labbayka Allahumma UmraNimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Umra Labbayka Allahumma HajjNimekuitikia Ewe Mola, (nimenuilia) Hajj TALBIYAH Labbayka-Llaahumma labbayk labbayka laa shariyka laka labbayk inna-l hamda wa-n ni'mata laka wa-l mulk, laa shariyka lak Tumeitikia Ewe Mola tumeitikia, Tumeitikia kwani huna Mshirika Tumeitikia, Hakika Himdi (shukurani) na Neema zote ni zako na Ufalme ni wako na huna mshirika. KUINGIA MSIKITINI Allaahumma salli `alaa muhammadin wa sallim, allaahumma aftah lee abwaaba rahmatika. Allah, Msalie muhammad na umfikishie salamu, O Allah nifungulie milango ya rehma zako.. KATI YA KONA YA YAMANI NA JIWE JEUSI Rabbanaa aatinaa fi-d dunyaa hasanatan wa fi-l aakhirati hasanatan wa qinaa 'adhaaba-n naar. Allah tunakuomba utupe yenye kheri katika dunia na yenye kheri akhera na utuepushe na adhabu ya moto. KUNYWA MAJI YA ZAMZAM Ibni Abdallah ibn Abbas alikuwa akiomba kwa kusemaAllahumma inni as’aluka I’lman naafian wa rizkan waasian wa shifa’an min kulli daainO’ Allah ninakuomba elimu yenye manufaa na riziki yenye kujitosheleza na shifaa kutokana na kila maradhi. SAFA NA MARWA Inna-s safaa wa-l marwata min sha'aa'iri-l llaahi faman hajja-l baita aw i`tamara falaa junaaha 'alaihi an yattawwafa bihimaa wa man tatawwa'a khairan fa inna-l llaaha shaakirun 'aleem. Hakika vilima vya Safa na Marwa ni katika alama za Allaah. Basi anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anayejitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Allaah ni Mwenye shukrani na Mjuzi.” ARAFAT "Laa ilaha illallaahu wahdahu laa shareeka lahu lahul mulk wa lahul hamdu wa huwa 'alaa kulli shay'in qadeer.” Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah pekee, hana mshirika, Ufalme wote ni wakeZ na himidi ( shukurani) zote ni kwake naye ni muweza wa kila jambo.
0
0
5
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Ummu Nasra  Kuna mambo mengi ya wazi kabisa ambayo sheria yameyakataza katika Uislamu na jamii imeghafilika nayo.  Mambo hayo huchangia  kuharibika na kuhatarisha mfumo  mzima wa kiislam ndani ya majumba. Miongoni mwa yenye kuhatarisha ni haya yafuatayo: 1. TELEVISHENI (TV) - LUNINGA.Televisheni kama inavyojuilikana (TV) ni chombo ambacho hakikosekani katika kila nyumba.  Kama kitatumika vizuri chombo hicho kwa mambo ya kheri yenye kuzidisha imani, kupeleka dini mbele, kukuweka mbali na maasi na kuhifadhi dini ya mja kinaweza kuleta faida.  Na kama kitatumika vibaya kinaweza kuathiri familia kwa asilimia kubwa kabisa.Ukweli ni kuwa kuangalia TV kuna madhara mengi na makubwa kuliko faida. Familia za kiislam zinaogelea kwa kasi kubwa bila ya kujali au kuona mabaya ya chombo hicho. Tuchukue mfano mdogo tu wa athari za televisheni kwa watoto kama utafiti huu mdogo uliofanyika hapa Uingereza unavyofafanua. Watoto wenye kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mawili kila siku wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa athma. Uchunguzi huo umeonyesha kuwa, kuangalia televisheni kwa muda mrefu kunaleta uwezekano wa kupata athma uongezeke mara mbili kwa watoto. Jinsi mfumo wa kupumua unavyofanya kazi wakati mtoto anapokaa tu bila kufanya chochote, hupelekea kutokea mabadiliko katika mapafu pamoja na magojwa mengine ya kupumua ikiwemo athma. Unene wa kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi kunakosababishwa na kuangalia muda mrefu televisheni hupelekwa kutokea hali hiyo Wataalamu wamesema kuwa, kuishi maisha ya kutokuwa na harakati yoyote katika umri mdogo hupelekea kuongezeka uwezekano wa hatari ya kupata athma ukubwani.Hivyo wamewashauri wazazi kuwashajiisha watoto wao kufuata maisha ya kawaida ya kuwa na mishughuliko na kupunguza muda wanaoutumia kuangalia TV. Wataalamu wa Uingereza wametoa taarifa hiyo baada ya kuwafanyia uchunguzi watoto 3,000  kuanzia wale waliozaliwa mpaka walio na miaka 11. Hasara moja ya kupoteza muda kuangalia TV inaweza kuzaa makosa mengi ndani yake.  Kuona na kusikiliza kuna wavutia wengi na kuwafanya watu kutawaliwa na tabia hiyo na kutoweza kuiepuka. Hakuna shaka kuwa jamii hasa watoto imeathirika sana na jambo hili.  TV inasababisha kwa kiasi kikubwa watoto wa Kiislamu kutumbukia katika tabia zisizo na maadili, ulevi, uzinzi, kukosa heshima, kujinasibisha na uzungu na mengi mengine maovu tunayoyaona katika jamii zetu.  Yote hayo wanayaona na kujifunza moja kwa moja kutoka kwenye TV.Mtu huhisi kuwa anapoteza wakati tu kujistarehesha na TV, anayakata masaa na dakika kwa ajili ya chombo hicho, ni makosa!!.  TV si chombo cha starehe, bali ni chombo kinachotumika kuchochea hisia, kubadilisha muelekeo na utiifu wa mtu. Na ndiyo hali halisi ndugu yangu Muislamu kama bado hujatanabahi.Yafaa Waislamu tuzinduke na kuziona faida chache na hasara nyingi za chombo hiki.  Kama tunaona ni neema hakika tutakuja kuulizwa namna tulivyoitumia.  [At-Takaathur 102:8] ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ - 102:8 Kisha mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa mlizitumiaje. Na kwa hakika hata  masikio na macho tunayoyatumia kwa chombo hicho pia tutakuwa ni wenye kuulizwa. Hivyo ni juu yetu kuchagua ni kipi cha kutizama. [Al-Israa 17:36].  وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا - 17:36 Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa Tv ni kama upanga ukiutumia vizuri unaweza kuleta faida na ukiitumia vibaya unaweza kuleta madhara makubwa.  Kwa mfano mtu akiweza kuidhibiti na kuangalia kwa nadra kwa vipindi vya kheri vyenye kwenda sambamba na dini yetu inaweza kukubalika, bali ni wachache wenye kufanya hivyo.  Wengi wao wameogolea na kuangalia tu bila hata ya kujali faida na hasara zake, na hii ndio iliopelekea madhara kuwa mengi kuliko faida.  Miongoni mwa madhara ya TV ni:- Kunapoteza wakati bure na kupuuza mengi ya wajibu- Inaeneza tamaduni za kikafiri kama ni njia moja ya kuigwa katika maisha- Inaeneza upotofu na uhuru kwa kupitia katika michezo, nyimbo matangazo yasiyo ya heshima ambayo hupelekea watizamaji kutumbuka na tabia hizo za kijinga.- Mazoea ya kuangalia TV yanaharibu akili na kuathiri afya ya mja. Hivyo kama kuna watu wazuri wenye kumuogopa Allah  Subhaanahu Wata’ala na kuonyesha mazuri yenye faida bila ya kukiuka mipaka ya Allah, basi unaweza kuangalia na ni jambo la kupendeza kwa wengi. Ni vyema kuchunga aina gani ya vipindi tunavyoangalia ndani ya majumba yetu.Ni wajibu wa kila mtu kueleweka wazi madhara na faida ya kifaa hichi ili tuweze kukitumia vyema ama kujiepusha nacho kabisa ikiwa tutashindwa kuweka vidhibiti katika majumba jinsi chombo hiki kitumike katika kunufaisha, kuelimisha na kuleta faida na si kuharibu, kupoteza muda na kupelekea jamii iliyozugika na hatimaye kupotoka na kupotosha wengine. Inaendelea IshaAllah.
0
0
6
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Ummu Nasra  UTANGULIZIHakika shukrani zote ni zake Allaah Subhaanahu Wata’ala, tunaemshukuru, tunaemtegemea, kumtaka msamaha na kutubu kwake. Tunajikinga Kwake Allaah Subhaanahu Wata’ala kutokana na shari za nafsi zetu na makosa ya matendo yake. Mwenye kuongolewa na Allaah hakuna wa kumpotoa, na mwenye kumpotoa hakuna wa kumuongoa. Rehma na Amani ziwe juu ya kipenzi chetu Muhammad SwallaAllahu ‘Alayhi wa Aalihi wa Sallam.‘Amma Ba’ad Nyumba ni neema kubwa ambayo mwanadamu amebarikiwa, وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ - 16:80 Na MwenyeziMungu amekujaalieni majumba yenu yawe maakaazi (yenu) [An-Nahl 16:80] Kuweka mazingira sahihi ndani ya majumba ni jukumu la kila muislam mume na mke, na ni lazima mazingira hayo yaoane sambamba na sheria alizotuwekea Allah Subhanahu wa Ta’ala. Moja kati ya njia ya kuyafikia hayo ni kuepukana na kila aina ya uovu na uharibifu ndani ya majumba. Kuna sababu nyingi kwa mwenye kuamini kuwa makini katika kuijenga na kuilinda nyumba yake katika misingi mema ya kiislam. Miongoni mwa sababu hizo ni: 1. Kujilinda yeye pamoja na familia yake kutokana na moto wa jahannam, na kujiweka mbali na ghadhabu zake. [At-Tahriym 66:6] يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ - 66:6 Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu na moto ambao ambao kuni zake ni watu na mawe 2. Kujua wajibu wake juu ya jukumu la kuchunga nyumba, na kujiweka tayari kujibu kwa kila unachokichunga. Hadith: Kutoka kwa Abdullah, Allah amuwie radhi, kwamba Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Aalihi wa Ssallamamesema: “Nyote ni wachunga na nyote mtaulizwa juu ya mlivyovichunga. Kiongozi anaewaongoza watu ni mchunga na ataulizwa juu wachungwa wake. Mwanamume ni mchunga kwa watu wake wa nyumbani na ataulizwa juu ya wachungwa wake. Na mwanamke ni mchunga kwa nyumba ya mumewe na watoto wake nae ataulizwa juu ya wachungwa wake .Mtumwa ni mchunga katika mali ya bwana wake na anawajibika juu ya mali hiyo. Hakika nyote ni wachunga na na kila mmoja wenu anawajibika juu ya wachungwa wake” Imesimuliwa na Bukhari na Muslim 3. Nyumba ni sehemu ya hifadhi kwa binaadamu, kujiweka mbali na kila aina ya ubaya na uovu ukiwa wa mnyama, binaadamu au majini, na kupata utulivu ndani yake. Amesema Mtume SwallaAllahu ‘Alayhu wa Ssallam: Usalama wa mtu katika wakati wa fitnah ni kubakia nyumbani kwake. Kilicho muhimu zaidi ni kuzingatia kuwa nyumba ni sehemu nyeti (muhimu) ya kujenga mazingira mazuri ya kiislam, kwani jamii bora hujengeka kuanzia nyumbani. Kwa masikitiko makubwa majumba yetu mengi yamejiweka mbali na mafundisho sahihi ya kiislam. InshaAllaah katika makala hizi tutaweza kugusia na kutanabahisha baadhi ya vitu ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika mfumo wa kiislam ndani ya majumba na jamii kwa ujumla, na kujaribu kutafuta njia muafaka kurejesha mazingira mazuri ndani ya majumba yetu. WabiLlaahi Attawfiyq InshaAllah itaendelea..
0
0
6
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Misingi ya sheria ni chimbuko la elimu yaani dalili na ushahidi wa jambo unapochukuliwa. Sheria yetu ya kiislamu imejiegemeza katika misingi mikuu mine. Miwili ikiwa ni mikuu na miwili ikiwa ni tegemezi kama ifuatavyo:QUR’AANSUNNAH (HADITHI)IJMAAQIYAAS QUR’AAN - MSINGI MKUU Ni msingi wa kwanza katika misingi mikuu . Kitabu chake Allah Subhaanahu Wata’ala alichomteremshia Mtume wake (Salla Llahu ‘Alayhi Wasallam) SUNNAH(HADITHI) - MSINGI MKUU Ni msingi wa pili mkuu. Sunnah - Hadithi katika sheria ni kila aliloliamrisha Mtume (Salla llahu ‘Alayhi Wasallam) au alilolikataza au alilolipendekeza katika kauli na vitendo na iqrari- kitendo cha Mtume(Salla Llahu ‘Alayhi Wasallam) kumuona mtu akitenda jambo na asitoe maelekezo yoyote ya kukemea au kukataza. IJMA’A - MSINGI TEGEMEZI Ijma’a ni kongamano na makubaliano ya wanazuoni wa kiislamu baada ya Mtume(Salla llahu ‘Alayhi Wasallam) juu ya jambo au suala ambalo halikuelezwa bayana ndani ya Qur’aan au Sunnah QIYAAS- MSINGI TEGEMEZI Qiyaasi ni mizani ya kulipima jambo au suala ambalo halina ufafanuzi ndani ya Qur’aan au Sunnah na jambo au suala lililotajwa, kwa kulingana sababu(Illa)zao. Imeitwa tegemezi kwa sababu ya kutegemea Quraan na Sunnah katika kulipatia hukumu jambo kwa ujumla . HUKUMU ZA SHERIA YA KIISLAMU Faradhi/WajibuManduub/SunnahHaramuMubah/HalaliMakruuh FARADHI/WAJIBU Fardhi au Wajibu ni jambo ambalo kila Mukallaf amelazimishwa na sheria kulitenda na jambo lenye limethibitika katika Quraan au Sunnah kwa dalili isiyo na shaka. MANDUUB/SUNNAH Jambo linalotatikana na sheria kulitenda kwa kila Mukallaf lakini bila ya kulazimishwa. Pia hujulikana kwa majina yafuatayo, Mustahab – jambo linalopendeza, Naafilah, Tattawu’u. Na miongoni mwa mambo ya Sunnah zipo za kawaida na nyengine zilizotiliwa mkazo. HARAMU Ni lile jambo lililokatazwa kwa mtazamo wa kisheria na kupata adhabu huko akhera tuendako au hapa hapa duniani kwa mwenye kulitenda. MUBAAH/HALALI Jambo lililoruhusiwa kisheria au kupewa khiari muislamu katika kulifanya au kutolifanya bila ya kutahadharishwa nalo au kupata dhambi au thawabu. Asili ya vitu vyote kwanza huwa Mubaah mpaka ipatikane dalili ya kuthibitisha vyenginevyo. Hakuna thawabu wala dhambi kwa kutenda/kutolitenda isipokuwa tu ikiwa halikufanyika linaweza kupelekea madhara kama mtu kukataa/ kugoma kula ataweza kulazimishwa kwa lengo la kuhifadhi nafsi MAKRUUH Jambo ambalo linachukiza - linalolikirihisha- kulitenda kwa mtazamo wa sheria. Hastahiki mtu kupata adhabu ya Mola kwa kulitenda bali akiacha atapata thawabu. MAQAASIDU SHARI’AH – MAKUSUDIO YA SHERIA Haya ni mambo ambayo sheria yetu ya kiislamu inatutaka tuyahifadhi na kuhakikisha tunayalinda kwa kuyatekeleza ipasavyo. 1 KUHIFADHI DINI- Kuhakikisha dini yeu inasimama katika ardhi na kuwa tayari kuilinda dini hii kwa ajili ya Allah Subahaanahu Wata’aala 2 KUHIFADHI NAFSI- Kuhakikisha haki ya kimsingi ya kila binadamu ya kuishi inatekelezwa na kuifanya haki hi iendelee katika ardhi kwa kutumia njia za halali (ndoa) katika kuongeza kizazi 3 KUHIFADHI AKILI- Kwa kuhalalisha kila chenye kuihifadhi akili na kuharamisha kila chenye kuleta madhara kwa akili kwani akili ni chimbuko la mambo yote ya kheri na moja katika mambo yanayoangaliwa kwenye kukalifishwa 4 KUHIFADHI KIZAZI- Ili kuweza kujenga jamii iliyo salama na madhubuti katika tabia na maadili na pia kuhakikisha kitakachohalalishwa katika maingiliano ya ndoa kimehalalishwa kwa mujibu wa sheria. 5 KUHIFADHI MALI- Mali ndio msingi wa kipato kwa mja hivyo ni wajibu kuhakikisha inahifadhiwa na kupatikana adhabu kwa walioifisidi SUNNAH Kilugha lina maana ya njia au mwenendo . Katika kulitafsiri neno hili na jinsi linavyotumika kisheria itabidi tuliangalie katika hali tofauti na maana zake ili tuweze kupambanua wakati linapotumika linakusudiwa kitu gani. SUNNAH KWA MTAZAMO WA KIHADITHI Ni kila kilichopokelewa kutoka kwa Mtume Salla llahu ‘Alayhi Wasallaam katika kauli ,vitendo , iqrari , sifa ya kimaumbile , sifa ya kitabia tokea kabla ya kupewa utume mpaka baada ya kupewa utume. Na katika maana hii neno sunnah na hadithi ni sawasawa SUNNAH KWA MTAZAMO WA KISHERIA Ni kila aliloliamrisha Mtume (Salla llahu ‘Alayhi Wasallam) au alilolikataza au alilolipendekeza katika kauli na vitendo na iqrari- [kitendo cha Mtume(Salla llahu ‘Alayhi Wasallam) kumuona mtu akitenda jambo na asitoe maelekezo yoyote ya kukemea au kukataza] Na jambo hili kutumika kama dalili katika hukumu ya kisheria. SUNNAH KWA MTAZAMO WA KIFIQH Ni kila jambo ambalo limethibiti kwa Mtume Salla llahu ‘Alayhi Wasallam lakini halipo katika hukumu ya fardhi wala wajibu. ISTWILAHI Maana ya neno kwa mtazamo wa kisheria.Mara nyingi maneno yana asili ya lugha ya kiarabu na hivyo kuwa na maana mbili moja ya kilugha – linavyojulikana neno kilugha na maana nyengine ya kiistwilahi – kisheria. Na maana hii ya kisheria ndio inayohitajika kutumika na kufanyiwa kazi.
0
0
15
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Imetayarishwa na Shani Ahmad Namshukuru Mwenyezi Mungu, ambae Ametuumba na Akatuweka katika ulimwengu ili tumuabudu Yeye pekee. Na Akatupa miongozo yenye kutuwezesha kuishi katika huu ulimwengu Aliotuumbia. Kisha Akatuletea wajumbe ili watufunze na kutubainishia miongozo hiyo ili tupate kuongoka. Napenda kuchukua nafasi hii, pia nakuomba na wewe msomaji kuchukua nafasi hii kumsalia Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), mbashiri wetu na muonyaji wetu. Kisha ningependa kuanza kwa kusema; Mwenyezi Mungu Mtukufu Alipotuumba akatuweka katika huu ulimwengu hakutuwacha tuu, bali alituwekea miongozo ambayo itaweza kutufikisha katika mafanikio ya upeo wa ubora wa maisha duniani. Akatuletea Mitume ili waje kutufunza na kutuongoza, Akawapa vitabu na sahifa zilizojaa uongofu na rehema Zake. Ili tupate mafanikio hapa duniani ni lazima tufuate miongozo hii itokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tuwafuate Mitume salawatu Llaahi wasalaamuhu ‘alayhim. Amesema Mwenyezi Mungu: “Na watahadhari wale wanaopinga amri zake (Mtume) itawapata fitnah au itawapata adhabu iumizayo.” [An-Nuur 24: 63] Amesema Ibn ‘Uthaymiyn katika Uswuul min ‘Ilmil-Uswuul, ‘kutokana na aya hii tunapata dalili ya kuwajibika twaa ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kwa vile Mwenyezi Mungu Anawahadharisha wale wanaopinga amri za Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa itawapata fitnah ambayo ni misukusuko katika maisha ya dunia au adhabu iumizayo huko Akhera. Maonyo kama haya hayaji ila kwa kuacha jambo la Wajibu, yaani ni kwamba amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pekee ni Wajibu kuitekeleza’. Endapo mwanaadamu ataacha kumtii Mwenyezi Mungu atakuwa ameacha kutekeleza Wajibu wake, hali ya kuwa amepinga amri ya Mola wake ya kumtii, hali hiyo itampelekea; Kwanza, kuingia katika dhambi ya uasi, ambayo Mwenyezi Mungu Ametuonya kwa adhabu kali ya moto kama Alivyosema katika Surat An-Nisaa: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا - 4:59 “Enyi Mlioamini mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wale wenye amri miongoni mwenu, na mtakapokhitilafiana juu ya jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa nyinyi ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho…” [An-Nisaa 4: 59] Aya hii imetuwekea ubainifu kwamba yule ambae hatorudisha khitilafu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume basi huyo si katika Waumini. Hali kadhaalika tunapata mafunzo kama haya katika Surat An-Nisaa: فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا - 4:65 “Si hivyo, naapa kwa mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe kuwa ndie hakimu juu ya yale yanayotokea miongoni mwao, kisha wasipate katika nafsi zao kipingamizi juu ya yale uliyohukumu na wajisalimishe kikamilifu.” [An-Nisaa 4: 65] Haya ni mafunzo kutoka Mola muumba yaliyo wazi yasiyo na shaka, yenye kututhibitishia kuwa twaa ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio mhimili mkuu wa iymaan zetu na Uislam wetu mafunzo haya ni ubainifu ulio dhaahir kuwa bila ya twaa iymaan zetu na kujisalimisha kwetu ni bure na vipi utakuwa Muislam yaani mwenye kujisalimisha ikiwa bado hutekelezi amri za yule unayedai kuwa umejisalimisha kwake? Tatu, kutokufanikiwa katika yale anayokusudia kuyafanya kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu katika Suurat Twaahaa: قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ - 20:123 ”Akasema tokeni humo nyote, (kutakuwa na) uadui miongoni mwenu, na ama pale utakapokufikieni kutoka kwangu uongofu, basi atakayefuata uongofu wangu huo, basi huyo hatapotea wala hatotaabika.” [Twaahaa 20 : 123] Katika aya hii kuna mazingatio makubwa, Mwenyezi Mungu Anatufahamisha kuwa hata baba yetu Nabii Aadam na mama yetu Hawwaa walipokiuka mipaka yake na kuacha twaa Yake, Aliwatoa katika pepo, pamoja na kuwa walitubu. Aya imeendelea na kutufunza kuwa tutakapokubali kufuata miongozo ya Mwenyezi Mungu hatutopotea wala hatutotaabika. Na mwenye kupuuza amri za Mwenyezi Mungu basi huyo atapata maisha dhiki na taabu hata kama atakuwa na utajiri wa mali na watoto, kwa kutotii amri za Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) mali yake na watoto wake watamtia katika dhiki ameahidi hivyo Mwenyezi Mungu katika Surat Twaahaa kwa kusema: وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ - 3:132 “Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa.” [Aali ‘Imraan 3: 132] Katika mafunzo ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ni kwamba hatoingia peponi ila yule aliepata Rehma za Mwenyezi Mungu, hivyo tukumbuke kuwa kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni jambo kubwa mno kwetu, ila kwa yule asie taka pepo katika maisha yake ya Akhera. Na katika kumtii Mwenyezi Mungu tunapata Uongofu kama Alivyosema katika Suuratun Nuur: 54: “na mkimtii mtaongoka” Na katika faida za kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni kupata utukufu wa kufufuliwa pamoja na watu wema waliohakikishiwa neema za Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, Masadiki, Mashahidi na Maswaalih. Kama Alivyosema (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Suurat An-Nisaa: تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ - 4:13 وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ - 4:14 “Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Yeye (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza katika Bustani zipitazo mito mbele yake; wakae humo milele. Na huko ndiko kufaulu kukubwa.” “na anayemwasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kuiruka mipaka Yake, (Mwenyezi Mungu) Atamwingiza Motoni, humo atakaa milele na atapata adhabu zifedheheshazo.” [An-Nisaa 4: 13-14] Ndugu zangu faida nyingi na hatuwezi kuzidhibiti zote katika makala hii, ni juu yetu kuzijua hivyo tufanye jitihada kuzitafuta ikiwa ni moja ya kutekeleza amri ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) ya kutafuta elimu. Inatupasa tukumbuke kuwa sisi ni Waislam na maana ya kuwa Muislam ni kujisalimisha au kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala), na kuyakubali yale yote aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kama ilivyopokelewa katika vitabu mbali mbali, amesema Abu Ja’afar At-Twahaawiy, katika ‘Aqiidat At-Twahaawiyyah, ‘Aqiydah namba 36, “Na Uislam wa mtu hautathibiti pasi na kujisalimisha na kujiweka chini ya nguvu za Mwenyezi Mungu...” Na kujisalimisha maana yake ni kuwa chini ya twaa ya Mwenyezi Mungu, kufanya kila Alilotuamrisha na kuwacha kila Alilotukataza, kumkusudia yeye tu katika ibada na mambo yetu yote ya maisha yetu. Ikiwa hatuwezi kuitimiza ahadi hii adhimu tuliyompa Mwenyezi Mungu ya kujisalimisha Kwake au kuwa tayari kutekeleza maamrisho Yake yote na kuyakubali yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) wapi tunashika katika kujivunia Uislam wetu? Maana Ya Sunnah Ni ufahamu wa wengi miongoni mwetu kuwa Sunnah ni vitendo au ibada ambazo tunapozitekeleza tunapata ujira, na tunapo yawacha hatutopata adhabu bali tutakosa ujira tu. Kutokana na ufahamu huu watu wengi wamejengeka na tabia ya kutotekeleza Sunnah na kusema ‘hiyo ni Sunnah tu si wajibu’, pale wanapotakiwa kutekeleza amri kati ya maamrisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Kwa hakika Sunnah ni mafundisho ya Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), ikiwa ni miongoni mwa maneno, vitendo au yale yaliyofanywa mbele yake nae akayakiri. Na juu ya haya ndipo tunalazimika kutekeleza Sunnah katika hali ya kuwajibika juu yetu kama ilivyobainishwa katika aya zilizokwisha tangulia hapo juu. Aya ambazo zinatuhimiza kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam). Hali hiyo ya kuwajibika kwetu katika Sunnah inaondoka pale tu Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) anapotubainishia, au kubainishwa na wanavyuoni kwa kufuata taratibu zake zinazokubalika. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Fiqh Kwanza kabisa tufahamu kuwa Sunnah ni neno la Kiarabu lenye maana ya njia ‘mwenendo’ yaani ni jambo ambalo limetokea kisha watu wakafuata mwenendo au jambo hilo. Kama ilivyopokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam): “Mwenye kuweka mwenendo mzuri basi atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakaofuata mwenendo huo, na mwenye kuweka mwenendo mbaya atapata ujira wa mwenendo huo na ujira wa watakao fuata mwenendo huo...” Hii ni maana ya Sunnah katika lugha. Ama katika matumizi ya Sunnah kwa wataalamu wa Fiqh, ni amali zilizo chini ya Waajib, zinakusanya kila kile ambacho Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amekipendekeza ambacho hakiwajibiki kukifanya. Sunnah kwa mtazamo huu hujulikana kama Manduub (mapendekezo) na hupata ujira mwenye kuzitekeleza na hatoingia makosani yule mwenye kuziacha. (M. H. Kamali, Hadith Studies) Na huu ndio mtazamo ambao wengi wetu tunaufahamu, mtazamo wa ki- Fiqh ambao umelenga katika kutoa hukumu za kishari’ah, na si maisha ya Wanaadamu ya kila siku kwa ujumla. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Hadiyth Vivile katika historia ya Dini, neno Sunnah limetumika kwa namna kadha, kwa mfano Wanachuoni wa Ahlul-Hadiyth, wanaitambua Sunnah ni chochote kile kilicho thubutu kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Semi zake , Matendo yake, Yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia, historia yake, Tabia na Maumbile yake. Baadhi ya Maulamaa wamewaita Wanachuoni wa Hadiyth ndio Ahlu-Sunnah. Baadhi ya Wanachuoni wakubwa wa karne ya tatu Hijriyyah waliandika vitabu kuhusiana na ‘Aqiydah na kuyapa majina As-Sunnah. Zama hizo watu walikuwa wanajulikana ni watu wa Sunnah kama ni katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah. Pia ilitumika kinyume cha Sunnah; Bid'ah (Uzushi) kwa kubainisha wale ambao si katika Manhaj sahihi ya ki-’Aqiydah. Sunnah Kama Inavyofahamika Kwa Wanachuoni Wa Uswuuliyyuun Amma Wanachuoni wa Uswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika. serifUswuliyyuun, wanaitambua Sunnah yakuwa ni sehemu kuu ya pili baada ya Qur-aan kuwa ndio chimbuko la shari’ah ya Dini yetu, hivyo Sunnah kwao ni Semi zote za Mtume Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), Matendo yake na yale yote yaliotendeka mbele yake na akayanyamazia. Na hii ndio maana halisi ya neno Sunnah inayopaswa itumike na kufahamika.
0
0
37
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Imekusanywa Na: Abu Faatwimah Makatazo yaliyothibiti maalumu kwa waumini wa kike ni kama yafuatayo: Katazo La Kuunganisha Nywele Tendo hili kwa huzuni kubwa limekuwa ni katika yenye kuonekana kuwa ni miongoni mwa mapambo, bali ni pambo lisiloepukika kwa kila mwenye kutaka kujiremba hasa kwa wenye kutaka kuolewa; wawe hawana nywele au wenye nywele ngumu/fupi au hata wenye nywele za singa; yote kutaka kuiga na kujifananisha na kudanganya, kwa kuwa tuko mbali na yaliyopokelewa kutoka kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kuunganisha nywele. Kutoka kwa Asmaa (Radhiya Allaahu 'anhaa) amesema: Alikuja mwanamke kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:"Ee Mjumbe wa Allaah! Hakika mimi nina binti ambae ni bibi harusi, amepatwa na maradhi –surua- hivyo nywele zake zimenyonyoka; je, niziunganishe?" Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Allaah Amemlaani mwanamke mwenye kuunganisha nywele na mwanamke mwenye kutaka kuunganishwa nywele" [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Al-Libaas, mlango wa mwenye kuunganishwa nywele, Hadiyth namba5515]. Na kutoka kwa bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kuwa palikuwa na mjakazi aliyeolewa miongoni mwa wanawake wa ki-Answaar, na huyo mjakazi alipatwa na maradhi yaliyopelekea kunyonyoka nywele zake, basi watu wake wakataka kuziunganisha nywele zake, wakamuuliza Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na kuunganisha nywele? Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia:"Amelaaniwa mwanamke mwenye kuunganisha nywele na mwanamke mwenye kutaka kuunganishwa nywele". [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Al-Libaas, mlango wa kuunganisha katika nywele, Hadiyth namba 5508 na 5509 na 5510]. Kwa hakika hichi kitendo cha kuunganisha nywele si miongoni mwa matendo yanayostahiki kutendwa na wenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah; kwani ni katika matendo na mitindo yenye kufanya na wasioamini Allaah na Siku ya Mwisho –wake kwa waume-, na hili liko dhahiri katika ulimwengu wetu; hivyo kwa mwanamke mwenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah kuunganisha nywele au kutaka kuunganishwa huwa anajifananisha na makafiri, na hilo limekatazwa kama ilivyopokewa kuwa Sa’iyd bin Musayyib amesema kuwa: “Alikuja Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Madiynah mara ya mwisho aliyokuja Madiynah akatuhutubia, basi akatoa donge la nywele [za bandia] akasema: Sikuwahi kumuona mtu yeyote anafanya haya isipokuwa Mayahudi; kwa hakika Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekiita kitendo hichi Az-Zuura: yaani mwenye kuunganisha nywele” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Al-Libaas, mlango wa kuunganisha katika nywele, hadiyth namba 5512; na Muslim, katika Kitabu cha Mavazi na Mapambo, mlango uharamu wa kitendo cha mwenye kuunganisha nywele na mwenye kutaka kuunganishwa, Hadiyth namba 3976]. Hadiyth hizi ziko wazi kabisa katika kuharamishwa kuunganisha nywele kama alivyosema al-Imaam An-Nawawiy na kulaaniwa kwa muunganishaji na mwenye kutaka kuunganishwa. Tendo hili -la kuunganisha nywele- ni katika madhambi makubwa kwa kumthibitikia Laana ya Allaah mwenye kufanya au kufanyiwa tendo hili; lakini kwa masikitiko makubwa kabisa juu ya kuthibiti Laana ya Allaah kwa watu hao [muunganishaji na mwenye kutaka kuunganishwa nywele] bado kuna wanawake wengi kabisa wenye kufanya tendo hili la kuunganisha nywele za wanawake wenzao au wenye kutafuta wa kuwaunganisha nywele kwa kisingizio cha kujiremba na kujipamba huku wakidai kuwa wao pia ni miongoni mwa wenye kumfuata na kumpenda Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni vyema ieleweke kuwa mwanamke akijipamba ikiwa si kwa ajili ya mumewe basi huwa haramu; na ikiwa atajipamba kwa ajili ya mumewe haitakiwi kujipamba au kujiremba isipokuwa kwa kilichohalalishwa na kukubaliwa na Shariy’ah ya Allaah; kwani haijuzu kwa mwanamke kujipamba kwa ajili ya mumewe kwa kitu Alichoharamisha au Alichokikataza Allaah. Katazo La Kujichora [Tattoo], Kunyoa Nyusi Na Kuchonga Meno Matendo haya matatu yote yamekatazwa; kwa kuthibiti laana kwa mwenye kuyafanya kwa kuwa ndani yake kuna kubadilisha maumbile ya Allaah. Matendo haya pia ni katika yenye kuonekana kuwa ni miongoni mwa mapambo na ni mtu kujitengeneza kwa namna atakavyo, kwa kuwa Muumba –wal –‘iyyaadhu bilLaahi- hakuwa na ufanisi wa kuwaweka vile watakavyo wenyewe katika kuwaremba kwa rangi na chapa tofauti iwe kwa mapicha zikiwemo za wanyama na kadhalika; huku wakisahau kuwa Muumba amesema: “Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa” [At-Tiyn 95: 4]. Mambo haya kwa baadhi ya ndugu zetu hasa waliobahatika kupata fursa ya kukutana au kuwaona makafiri yamekuwa ni uthibitisho wao wa kuwathibitishia wengine kuwa wao waliwahi kufika Ulaya na katika waliyoyaona ni huku kujichora, kujipiga chapa na kadhalika. Msiba huu wa kujiremba na kujichapa kwa kijichora umewasibu pia baadhi ya waliojaaliwa kuwa wanaume, yote kwa kuwa hawana shukurani kwa kuumbwa waume wala hawaelewi thamani yake; hivyo kwa kupenda kuiga na kujifananisha mtu hujisahau mpaka akafikia kutojikumbuka kuwa umbile lake lilikuwa namna ipi. Kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) amesema kuwa: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanamke mwenye kuunganisha nywele na mwanamke mwenye kutaka kuunganishwa nywele, na mwanamke mchanjaji [mwenye kuwachanja wanawake wenzake kwenye sehemu yoyote ile ya mwili] na mwanamke mwenye kutaka kuchanjwa.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Al-Libaas, mlango wa mwenye kutaka kuchanjwa, Hadiyth namba 5511, 5514,5516 na 5521]. Ama kunyoa au kunyolewa nyusi ni janga jengine; kwani imekuwa ni katika mapambo kwa kila mwenye kutaka kujiremba hasa kwa wenye kutaka kuolewa. Na kutokana na 'AbdullAah bin Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba: “Allaah Amewalaani wanawake wenye kuwachanja wenzao [tattoo], na wanawake wenye kuchanjwa, na wanawake wenye kuwanyoa wenzao nyusi na wanawake wenye kunyolewa nyusi; na wanawake wenye kuchonga meno kwa urembo [kutengeneza mwanya wapate kuonekana kama ni wasichana, kwa kuwa mwanya hupendeza kwa wasichana] kwa ajili ya kujipamba; wanawake wenye kubadilisha maumbile ya Allaah”; akasema: Hadiyth hii ikamfikia mwanamke kutoka Bani Asad aliyekuwa akiitwa kwa jina la Ummu Ya’quub, mwanamke huyu alikuwa msomaji wa Qur-aan, aliposikia Hadiyth hii alikuja kwa Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) na kumwambia kuwa: “Kilichonileta kwako ni Hadiyth niliyofikishiwa kuwa wewe umewalaaani wanawakewenye kuwachanja wenzao na wanawake wenye kuchanjwa; na wanawake wenye kuwanyoa wenzao nyusi na wanawake wenye kunyolewa nyusi; na wanawake wenye kuchonga meno kwa ajili ya urembo; na wanawake wenye kubadilisha maumbile ya Allaah”; yule mwanamke akamuuliza kuhusu jambo hili? Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) akamwambia:"Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah!. Yule mwanamke akasema: “Kwa hakika nimesoma baina ya magamba mawili ya msahafu [Kitabu cha Allaah chote kwa ukamilifu] mbona sijakutana na hilo?!” Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) akamwambia: “Kama ulikisoma kwa ukamilifu basi bila ya shaka yoyote ile ulikutana na hilo; Allaah Aliyetukuka Amesema:“Na anachokupeni Mjumbe chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho” [Al Hash-r 59:7]. Yule mwanamke akasema: “Hakika mimi naona kuna jambo kama hili kwa mkeo hivi sasa; Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) akamwambia: “Nenda ukaangalie vyema”, Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) akasema: “Yule mwanamke aliingia ndani kwa mke wa 'Abdullah lakini hakuona kitu alichodai kuwa anacho huyo mke wa Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu)”; yule mwanamke akasema: “Sikuona kitu”; Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu 'anhu) akasema: “Na kama angekuwa anacho hicho ulichodai kuwa anacho basi nisingelimuingilia” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Tafsiyr Qur-aan, Suuratul Hashr, Hadiyth namba 4534; na katika kitabu cha al-Libaas, mlango wa mwanamke mwenye kutaka kuchanjwa, Hadiyth namba 5522; na mlango wa wanawake wenye kunyoa nyusi, Hadiyth namba 5506, 5513 na 5517; na Muslim, katika Kitabu cha Mavazi na Mapambo, mlango uharamu wa kitendo cha mwenye kuunganisha nywele na mwenye kutaka kuunganishwa, Hadiyth namba 3973]. Na kutoka kwa Abu Juhayfah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: “Amekataza Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) [Kutumia] thamani ya damu, thamani ya mbwa, pato la mhasharati; na amemlaani mwanamke mwenye kuwachanja wenzake na mwanamke mwenye kutaka kuchanjwa; na mla ribaa na wakala wake; na mchora picha” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Hajj, milango ya Muhswar na jaza ya Swayd [kuwinda], Hadiyth namba 2095; na katika kitabu cha Al-Libaas, mlango wa mwenye kuchanja, Hadiyth namba 5519.; na katika Kitabu cha Tafsiyr Qur-aan, Suurat Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 5535]. Matendo haya yote –kujipiga chapa, kunyoa nyusi na kuchonga meno- ni haramu kwa mtendaji na mwenye kutaka kutendewa kutokana na Hadiyth hizo, na pia matendo hayo yote ni katika yenye kueleweka kuwa ni kubadilisha maumbile ya Allaah, na ni udanganyifu. Kuthibiti Laana ya Allaah kwa mwenye kufanya au kufanyiwa matendo haya inathibitisha kuwa matendo hayo ni katika madhambi makubwa pia, lakini kwa masikitiko makubwa kabisa bado kuna wanawake tena wengi sana wenye kutaka kuolewa hufanya matendo haya au hufanyiwa; ili wadhaniwe kuwa ni wasichana wadogo au wadhaniwe kuwa ni wenye nyuso nzuri na za kuvutia; la kusikitisha na kuhuzunisha zaidi ni kule kwa baadhi ya kina mama kuwapeleka wasichana wao wadogo kufanyiwa matendo haya. Huenda likazuka suala hapa; je wale wanawake wenye kuota ndevu au masharubu inaruhusiwa kwao kuzinyoa au kuyanyoa? Jawabu: Naam, inajuzu kwa wanawake kama hawa kuzinyoa ndevu zenye kuota katika nyuso zao au masharubu; na wala hawaingii katika laana; bali kwa kuzinyoa hizo ndevu na hayo masharubu watakuwa wanatekeleza agizo la Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) la kuwataka wanawake wasijifananishe na wanaume, na kwa wanawake kama hawa hawana njia ya kutojifananisha na wanaume isipokuwa kunyoa hizo ndevu au hayo masharubu; na watakapoziacha hizo ndevu au hayo masharubu watakuwa wamejifananisha na wanaume na huko ndiko kwenda kinyume na agizo la Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Pia ikiwa mwanamke atahitaji kuchonga meno yake kwa sababu za kimatibabu au kuondosha aibu katika meno; mwanamke huyu haingii katika laana wala kufanya hivyo haitokuwa haramu kwake kwa kuwa neno “...kuchonga meno kwa urembo” lililotumika katika Hadiyth linaonyesha wazi kuwa uharamu uko kwa mwenye kuchonga kwa ajili ya kutafuta urembo na uzuri, hivyo wakati wowote ule atapohitajia mwanamke kuchonga meno yake kwa ajili ya kimatibabu huwa hana dhambi, Allaahu A‘alam. Katazo La Kutoka Nje Huku Akiwa Amejitia [Ananukia] Manukato Moja katika madai ya wanawake ni kuwa mtu si vizuri kusikiwa harufu mbaya [majasho]; juu ya kuwa kuna waume ambao hawasikia harufu nzuri za wake zao isipokuwa pale wanapotoka kwenda katika maharusi; katika kulidhibiti hilo huwa wanapotoka kwa kutaka kutimiza mahitajio yao, kwenda shughulini au shughuli zao za kawaida hujitia manukato yenye kuhanikiza, udi, mafuta mazuri, mafuta ya nywele yenye kunukia au mafuta ya kujipaka mwilini yenye kunukia au hata wanapokoga hutumia sabuni zenye kunukia ili wawe na harufu wanapotoka; desturi hii inawapeleka wengine kushikamana nayo hata wanaposaidiwa kupelekwa pahala kwa gari iwe ya kulipa au ya rafiki wa mume [akiwa na huyo mume mwenyewe ndani ya gari] au hata kwenda Misikitini hujimwagia manukato na kusikiwa na kila mtu awe mpita njia, dereva, na kadhalika. Kwa anayeelewa basi huu ni msiba, na msiba huwa mkubwa zaidi kwa asiyeelewa; kwani jamii yaonyesha kuwa si kuwa iko mbali tu na mafundisho aliyokuja nayo Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), bali jamii imeyatupa mbali na kuyadharau mafundisho na kila lenye kuambatana na mafundisho hayo. Kutoka kwa bibi Zaynab ath-Thaqafiyyah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: "Atakapo shuhudia mwanamke mmoja wenu Swalah ya 'Ishaa [na katika riwaayah: Msikitini] basi asiguse manukato usiku huo” [Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Swalah, mlango wa kutoka wanawake kwenda Misikitini ikiwa haitosababisha fitnah na hali yeye..., Hadiyth namba 678 na namba 679]. Na kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ”Mwanamke yeyote yule ataejifukiza udi [harufu nzuri] basi asishudie pamoja nasi Swalah ya ‘Ishaa ya mwisho” [Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Swalah, mlango wa kutoka wanawake kwenda Misikitini ikiwa..., Hadiyth namba 680.] Na kutoka kwa Abu Muusa Al-Ash-‘ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ”Mwanamke yeyote yule ataejitia manukato akapita mbele ya watu ili waipate harufu yake basi huyo ni mzinifu [atakuwa amezini]” [Imepokelewa na Ahmad katika musnad wake, kitabu Musnad wa watu kumi waliobashiriwa pepo, hadiyth ya Abi Musa Al-Ash-‘ariy (Radhiya Allaahu 'anhu), Hadiyth namba 19272 na 19305; na at-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Adabu, mlango wa yaliyokuja katika yenye kuchukiza kutoka kwa mwanamke ..., Hadiyth namba 2730]. Hadiyth hizi zote dada yangu katika iymaan zinathibitisha uharamu wa kutoka nyumbani kwako hali ya kuwa unanukia, kwani manukato au harufu yake haraka huwafanya wanaume wavutiwe na kupata matamanio ya kutaka kumkaribia aliyejipaka hayo manukato. Katika kusherehesha neno [huyo ni mzinifu] Wanazuoni wanasema kuwa “Amezini kwa kuwa amesababisha kuzindua matamanio ya wanaume kwa hiyo harufu wanayoipata inayotokana na manukato [au udi] aliyojitia; jambo linalowapelekea kutaka kuelewa nani huyo mwenye kunukia na hilo huwapelekea kumkodolea macho; na mwenye kumtazama huwa amezini [zinaa ya macho], kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ameandikiwa kila mwanaadamu sehemu yake katika zinaa; hakuna njia ya kuiepuka; macho mawili zinaa yake ni kutazama, masikio mawili zinaa yake ni kusikiliza, na ulimi zinaa yake ni kusema, na mkono zinaa yake ni kuunyoosha, na mguu zinaa yake ni hatua zake, na moyo hupata matamanio, na tupu husadikisha au kukadhibisha” [Imepokelewa Al-Bukhaariy, katika Kitabu cha Tafsiyr Qur-aan, Suurat Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 6152; na Muslim, katika Kitabu cha Qadar, mlango wa imekadiriwa juu ya kila mwanaadam sehemu yake katika zinaa, Hadiyth namba 4808 na namba 4809]. Ni jambo linaloeleweka kuwa kumtazama mwanamke ni katika vitangulizi vya zinaa ya sehemu za siri za wanaume, hivyo ni wajibu kwa kila dada mwenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah kutotoka nyumbani kwake isipokuwa kwa haja [dharura] yenye kukubalika na Shariy’ah, na hapo atapohitaji kutoka, basi ahakikishe kuwa anajipamba kwa adabu za kishariy’ah ambazo miongoni mwake ni kuwa amejifunika na kujisitiri vizuri kwa hijabu ya kishariy’ah; na wakati wowote ule ataporudi nyumbani kwake yuko huru kujitia manukato atakavo, kwa sharti kuwa hawatoipata harufu ya manukato yake wanaume wengine wasio kuwa maharimu zake. Katazo La Kudhihirisha Mapambo Kwa Wanaume Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijaahiliyyah...…” [Al-Ahzaab 33: 33]. Amesema Mujaahid: “Walikuwa wanawake wanapotoka nje ya nyumba zao hujipitisha mbele za wanaume, na huko ndiko kujishauwa kwa majishauwo ya kijaahiliyyah.” Amesema Qataadah: “Walikuwa wanawake wanapotoka nje ya nyumba zao, hutembea ovyo pasina hayaa na huku wakijitikisa tikisa, na ndio Allaah Aliyetukuka Akawakataza.” Amesema Muqaatil bin Hayyaan: “Tabarruj ni pale mwanamke anapokuwa ameweka Khimaar [shungi] kwenye kichwa chake lakini akawa hakuifunga itakiwavo, hivyo mkufu [kidani], vipuli [herini], shingo yake na vyote hivyo vikawa vinaonekana”. Wanawake wanakatazwa kujishauwa na kujitikisa tikisa wakati wakiwa wako nje ya nyumba zao; na huwa ubaya zaidi pale wanapokuwa wamejipamba kwani kutawapelekea wanaume wawatazame na kuyaona mapambo yao; wanawake hawa huwa na mitindo ya kimaajabu ya kupiga viatu vyao chini na kadhalika. Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa Motoni sijawahi kuziona: Watu ambao wana fimbo [mijeledi] kama mikia ya ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi; wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao [kwa kuwa warahisi]; vichwa vya wanawake hao kama nundu za ngamia zinazoyumba; hawatoingia Peponi na wala hawatoipata [hawatosikia] harufu yake, na harufu yake inaweza kusikiwa kutoka masafa kadhaa na kadhaa” [Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Jannah na sifa za na’iyma zake na watu wake, mlango wa Moto watauingia majabari na Pepo wataiingia madhaifu, Hadiyth namba 5103; na katika Kitabu cha Mavazi na mapambo, mlango wa wanawake Al-Kaasiyaat Al’Ariyaat Al Maailaati.., Hadiyth namba 3978]. Angalia dada yangu katika iymaan makemeo makali hayo na mazito na adhabu inayomsubiri mwenye kujifakharisha kwa uzuri wake na kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume wasio kuwa maharimu zake; huenda kwa mwanamke kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume hapa duniani ikawa furaha, fakhari, pato zuri [kama wenye kushiriki katika mashindano ya mwanamke mzuri] tija na umaarufu; lakini itakuwa hasara na majuto Siku ya Qiyaamah, kwani itakuwa ni sababu tosha kwa yeye kujiharamishia Jannah na kutumbukizwa Motoni. Ewe mwenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah! Jihadhari na kudhihirisha mapambo yako kwa wanaume wasiokuwa maharimu zako; jihadhari sana na kutojisitiri vizuri kwa hijabu ya kishariy’ah utokapo nje ya nyumba yako, au hata ndani ya nyumba yako wakiwepo wasiokuwa maharimu zako; jihadhari na kujitia manukato, udi na mfano wa hivyo wakati unapotoka nje ya nyumba yako; jihadhari na kupatikana harufu ya manukato yako na wanaume wasiokuwa maharimu zako; yote hayo dada yangu katika iymaan ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako na ni katika yenye kukupelekea kuwa miongoni mwa wenye kuwajibikiwa adhabu Siku ya Qiyaamah.
0
0
36
Al-Iman
Aug 04, 2018
In Masomo
Imekusanywa na Shani Ahmad Bismillahir Rahmaanir RahiymAlhamdulilLlaah, was swalaatu wa salaam ‘alaa Muhammadin (Salla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).Anapokuwa Katika Hali Ya Kutoka Roho· Wanaohudhuria mauti ya Muislam wanatakiwa wamlakinie Shahadah.Yanapobainika Mauti Yake· Kumfumba macho.· Kulainisha viungo vyake ikibidi.· Kumvua nguo zake.· Kumuweka kitandani.· Kumuombea Du’aa. Kumfunika. Kuanza matayarisho ya maziko. Yanayojuzu Kwa Wanaohudhuria Kumfunua uso na kumbusu. Kulia pasina kunung’unika na kuomboleza au kuchupa mipaka. Yanayowapasa Watu Wa Karibu Ya Maiti Pindi Wanapopata Habari Za KufiliwaKusubiri na kuridhia Qadhaa ya Mwenyezi Mungu na asome du’aa hii: “Hakika sote tunatoka kwa Allaah, na Kwake sote tutarejea, Nakuomba Allaah unipe ujira katika msiba wangu huu na unifidie na kilicho bora zaidi.” Yaliyoharamishwa An-Niyaahah nako ni kuomboleza kwa kunung’unika na kupiga kelele (kunaongeza huzuni na kuondosha subira, na kujikubalisha na Qadhaa ya Allaah). Kuchana nguo. Kunyoa nywele. Kukosha Maiti Hukumu yake ni Fardhi Kifaayah. Siqtwi (kilichoanguka; kiumbe kilichoharibika tumboni kwa mama yake) huoshwa ikiwa ni baada ya miezi minne. Shahidi wa uwanja wa mapambano haoshwi hata akiwa na Janaba Si fardhi kuosha maiti ya kafiri, bali inajuzu kwa Muislam kumousha jamaa yake akiwa miongoni mwa makafiri. Walio bora kuosha maiti ni familia yake. Inajuzu mume kumuosha mke na kinyume chake. Anapofariki mwanamke miongoni mwa wanaume, na mwanamme miongoni mwa wanawake, na pakakosekana muoshaji wa jinsia ile. Kwa hali kama hiyo inapotokea, maiti hutayamamishwa. Wanaume watamtayamamisha mwanamke na Wanawake watamtayamamisha mwanamme hali ya kuwa maiti yupo na nguo zake. Sifa Za Muoshaji Muoshaji kuwa na sifa njema na usiri. Kuwa na elimu ya kuosha Faida: inajuzu mwenye hedhi au mwenye janaba kuosha maiti kwa vile hakuna dalili inayokataza.Namna Ya Kukosha Maiti Huoshwa mara tatu au tano au saba… Kwa maji na majani ya mkunazi (sabuni), na josho la mwisho lichanganywe na kaafuur. Mwanamke afumuliwe nywele zake. Zisukwe tena mikia mitatu baada ya kuoshwa na kutupwa nyuma yake na si kifuani kwake. Kuwepo na upole na huruma Muoshaji anaanza kwa kumchua tumbo kwa upole kutoa uchafu ulio baki. Kumtawadhisha Wudhuu wa Swalah. kumuosha kichwa na shingo pamoja na ndevu. Amuoshe upande wa kulia kuanzia shingoni mpaka kwenye kisigino na upande wa nyuma. Upande wa kushoto kama alivyofanya upande wa kulia. Atakaushwa maji. Yatakapokosekana maji atatayamamishwa. Atakapozikwa bila ya kukoshwa atafukuliwa endapo hajaharibika. Faida: Mwenye hedhi au janaba huoshwa josho moja tu kwa vile hukumu za kishari’ah hazimuwajibikii tena. Na mwenye kukosha maiti haimuwajibikii kukoga; akipenda ataoga, akipenda atanawa mikono yake.Kumkafini Kumkafini maiti ni Fardhi Kifaayah. Kafani inunuliwe kutokana na mali ya maiti. Inajuzu kujinunulia kafani kabla ya mauti. Sifa Ya Kafani Ya mwanamme (na hata ya mwanamke) ni shuka tatu. Inapendeza ziwe nyeupe. Inapendeza ziwe za pamba. Iwe safi na yenye kusitiri. Itiwe manukato. Mwenye kuhirimia mashuka mawili na asifunikwe kichwa. Shahidi kafani yake ni nguo zake alizofia nazo. Ya mwanamke ni kama ya mwanamme. Imezoeleka mwanamke vipande vitano vya nguo lakini Hadiyth inayofundisha hivyo si sahihi, hivyo ni bora kushikamana na mafunzo sahihi yanayoonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya mwanamme na mwanamke katika kafani japokuwa kuna baadhi ya Wanazuoni wamependekeza hivyo. Baada Ya Maziko Kulipa madeni yake haraka. Kutoa pole (taazia) kwa kusema: "Hakika ni cha Allaah Alichokichukua na ni Chake Alichokitoa, na kila kitu mbele Yake kina muda maalum, hivyo subiri na utaraji malipo.” Haya ndio tuliyojaaliwa kutoa katika Sunnah na Allaah Ndie Mjuzi zaidi.
0
0
14